單集摘要
Mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa uchumi na maisha ya mamilioni ya watu barani Afrika, cha kushangaza ni kwamba, licha ya Afrika kuchangia kwa kiwango kidogo katika uzalishaji wa hewa chafu duniani, hali hii imezifanya nchi za Afrika kutoa wito kwa mataifa tajiri kutoa fedha za ufadhili kama ruzuku badala ya mikopo ili kufanikisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Lakini je, kwa nini Afrika inasisitiza msimamo huu?
Mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa uchumi na maisha ya mamilioni ya watu barani Afrika, cha kushangaza ni kwamba, licha ya Afrika kuchangia kwa kiwango kidogo katika uzalishaji wa hewa chafu duniani, hali hii imezifanya nchi za Afrika kutoa wito kwa mataifa tajiri kutoa fedha za ufadhili kama ruzuku badala ya mikopo ili kufanikisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Lakini je, kwa nini Afrika inasisitiza msimamo huu?
單集
Ufadhili wa Tabianchi: Kwa nini Afrika inataka ruzuku badala ya mikopo?
已收聽Mabadiliko ya tabianchi yanaendelea kuwa tishio kubwa kwa uchumi na maisha ya mamilioni ya watu barani Afrika, cha kushangaza ni kwamba, licha ya Afrika kuchangia kwa kiwango kidogo katika uzalishaji wa hewa chafu duniani, hali hii imezifanya nchi za Afrika kutoa wito kwa mataifa tajiri kutoa fedha za ufadhili kama ruzuku badala ya mikopo ili kufanikisha mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabianchi. Lakini je, kwa nini Afrika inasisitiza msimamo huu?
Mkutano wa Urusi na Afrika, Moscow inatafuta nini kwa bara hili?
已收聽Mwezi uliopita viongozi kutoka Afrika walisafiri hadi Moscow Urusi kwa mkutano uliolenga kuimarisha ushirikiano baina ya bara hilo na Urusi, hata hivyo swali ambalo watu wengi wanajiuliza ni kwanini Afrika ni kama ina iamini sana Urusi? Tumezungumza na Francis Ibrahim, mtaalamu wa masuala ya diplomasia.
Gazeti linapogeuzwa kuwa penseli ya kuandikia
已收聽Msikilizaji, je, wajua kuwa gazeti la zamani linaweza kugeuzwa kuwa penseli na wakati huo huo kutoa ajira kwa vijana? Huo ndio ubunifu wa wajasiriamali wawili katika eneo la Athi River nchini Kenya ambao wamegeuza magazeti yaliyotumika kuwa fursa ya biashara na chanzo cha kujikimu kimaisha.
DRC: Ufugaji wa nyuki unavyokwamua maisha ya raia wa mji wa Goma
已收聽Mji wa Goma, mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, unaendelea kukabiliwa na changamoto za kiusalama na kiuchumi, huku ukiwa chini ya udhibiti wa waasi wa FRN wanaoongozwa na rais wa zamani Josephu Kabila, ambako fursa za ajira ni chache na vijana wengi wanakabiliwa na changamoto ya kujipatia kipato, hata hivyo baadhi yao wameamua kutafuta njia mbadala za kujikimu na kusaidia familia zao.
Afrika kuzindua taasisi ya ukadiriaji mikopo, je itasaidia?
已收聽Afrika imezindua rasmi Wakala wa Ukadiriaji wa Mikopo wa Afrika, Africa Credit Rating Agency (AfCRA), hatua inayolenga kushughulikia changamoto za gharama kubwa za mikopo na kuvutia uwekezaji zaidi kwa ajili ya maendeleo ya bara hilo. Je, kuanzishwa kwake kutapunguza kweli gharama za mikopo kwa mataifa ya Afrika, au ni mwanzo tu wa safari ndefu ya mageuzi ya kifedha?